VISA | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 VISA

Utangulizi:

Visa ni kampuni inayoongoza katika teknolojia ya malipo duniani inayowawezesha wateja, wafanyabiashara, benki na serikali kutumia pesa kidigitali. Muungano kati ya Tigo na VisaNet unarahisisha huduma ya ufanyaji wa miamala ya benki kwenda Tigo Pesa kwa kuwawezesha wateja kutoa pesa kutoka kwenye akaunti zao za benki moja kwa moja.

Bidhaa hii mpya ina huduma mbambali kama ifuatavyo.

 1. Kuziunganisha kadi za debit/credit/prepaid na akaunti zao za Tigo Pesa
 2. Kutuma pesa kwenda akaunti ya Tigo Pesa kutoka kwenye kadi ya Visa
 3. Kufanya marekebisho ya Kadi
 4. Kufunga na Kufungua kadi
 5. Kuondoa kadi kwenye mfumo

Faida:

Faida kubwa za huduma ni;

 • Ni ya Uhakika, kwa kutumia huduma hii mteja anaweza kutoa pesa wakati wowote na mahali popote kwa kutumia App ya Tigo Pesa.Hakuna haja tena ya kwenda kwenye ATM za VISA ili kutoa pes ana kuweka kwenye akaunti ya Tigo Pesa.
 • Ni Rahisi, hauhitaji kutumia Menyu ya benki kufanya miamala ya benki kwenda Tigo Pesa, kila kitu kinafanyika moja kwa moja.

Bidhaa hii itawawezesha wateja wenye kadi za VISA kutoa pesa kutoka benki kwa urahisi zaidi kwa kutumia App ya Tigo Pesa.


Jinsi ya Kuunganisha Kadi:

Fungua App ya Tigo Pesa >>Huduma za Kifedha>>Chagua VISA>>Chagua Unganisha Kadi>>Kubali>>Ingiza taarifa za kadi>>Ingiza namba ya siri>>Hakiki taarifa>>Taarifa ya Uthibitisho.

Jinsi ya Kutuma Pesa:

Fungua App ya Tigo Pesa >> Huduma za Kifedha >> VISA >> Kutuma Pesa>>Chagua kadi >> Ingiza kiasi na maelezo ya muamala(sio lazima) >> Ingiza CVV (namba tatu zilizoko nyuma ya kadi) >> Ingiza namba ya siri ya tigo Pesa>> Ujumbe wa Uthibitisho.

Fungua App ya Tigo Pesa >> Huduma za Kifedha >> VISA >> Kutuma Pesa>>Chagua kadi >> Ingiza kiasi na maelezo ya muamala(sio lazima) >> Ingiza CVV (namba tatu zilizoko nyuma ya kadi) >> Ingiza namba ya siri ya tigo Pesa>> Ujumbe wa Uthibitisho.

Jinsi ya Kuondoa Kadi:

Fungua App ya Tigo Pesa >>Huduma za kifedha>> VISA >> Mpangilio (Setting) wa kadi >> Ondoa kadi>> Chagua namba ya kadi >> Chagua Kujiondoa >> >> Ujumbe wa Uthibitisho.

 

Maswali na Majibu:

  Nawezaje kuunganisha kadi ya VISA nan amba ya Tigo Pesa?

Wateja wa TigoPesa anaweza kuunganisha kadi yake namba ya kadi ya visa kwa kutumia App ya Tigo Pesa.

  Je, kuna gharama zozote za kuunganisha na kuondoa kadi ya VISA?

Hakuna gharama zozote wakati wa kuunganisha na kuondoa kadi ya Visa kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa.

  Je, huduma hii inapatika kwenye menyu ya Tigo Pesa (*150*01#)?

Ndio, huduma hii inapatikana kwenye App ya Tigo Pesa na kwenye Menyu ya Tigo Pesa pia

  Ni kadi ngapi za Visa mteja anaweza kuziunganisha?

Mteja anaweza kuunganisha hadi kadi 3 za visa na akaunti yake ya Tigo Pesa.

  Nafanyeje ili kuondoa kadi ya Visa kupitia App?

Fungua App ya TigoPesa >> Chagua Huduma za kifedha >> Chgua VISA >> Mpangilio (Setting) wa  >> Ondoa kadi.

  Je, mteja anaweza kumuunganisha mteja mwingine wa Visa na akaunti yake ya Tigo Pesa.

Hapana, kila mteja anatakiwa kuwa na taarifa kamili na mmiliki halali ili kuunganisha kadi yake.

  Kuna utofauti gani kati ya kuondoa kadi na kufunga kadi?

Kuondoa kadi ina maana kwamba mteja kwa maamuzi yake ameamua kuondoa taarifa za kadi  kwenye mfumo moja kwa moja.

Lakini

Kufunga kadi ina maana kwamba mteja kwa makusudi ameamua kuzuia kwa muda matumizi ya kadi hadi pale atakapoifungua tena.

  Kuna makato yoyote ya kutuma pesa kutoka benki kwa kutumia VISA? Ni kiasi gani?

Ndio,kuna gharama za kutuma pesa kutoka benki lakini kiasi kinatofautiana kutokana na benki unayotumia.

  Ni akaunti ngapi za Tigo Pesa zinaweza kuunganishwa na kadi moja ya VISA?

Akaunti moja tu ya TigoPesa inaweza kuunganishwa na kadi ya Visa.

  Huduma hii inapatikana kupitia benki zipi?

Kwa sasa;huduma hii inapatikana kupitia benki zilizosajiliwa kwenye Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

  Je, mteja anatakiwa afanye nini anapoona ujumbe wa kuomba uthibitisho wa Visa anapojaribu kuunganisha kadi yake ya Visa?

Kwa kila ujumbe wa kuomba uthibitisho mteja anatakiwa kufika kwenye benki husika kwa msaada zaidi.

  Endapo ikitokea kukwama kwa huduma au mahitaji ya msaada ni nani wa kuwasiliana naye?

Endapo unashindwa kupata huduma au unahitaji msaada, tafadhari piga namba 100 kwa msaada zaidi.

Vigezo na Masharti:

 

 1. MTEJA:
  • Bidhaa hii inaweza kutumiwa na mteja yeyote kutoka kwenye mtandao wowote wa simu.
  • Ada za malipo kwa wateja wa mitandao mingine zitakua kama zilivyowekwa na mtandao husika.
  • Wateja wataweza kufanya malipo yasiozidi Milioni 5 za Kitanzania.
  • Tigo haitashiriki kwenye makubaliano yoyote kati ya mfanyabiashara na mteja.

 

 1. MFANYABIASHARA

  Nyaraka zinazohitajika ili kusajiliwa kwenye huduma:

  Kwa Wafanyabiashara wa kati

  • Cheti cha TIN
  • Leseni ya biashara
  • Namba ya Tigo iliyosajiliwa
  • Cheti cha Brela (Kama unataka kubadili jina lako na kuweka la biashara)

 

 1. Kwa Kampuni/Taasisi:
  • Cheti cha TIN
  • Leseni ya biashara
  • Namba ya Tigo iliyosajiliwa
  • memorandum and article of association
  • Barua ya utambulisho

 

 1. Kwa Machinga
  • Kitambulisho cha Machinga
  • Namba ya Tigo iliyosajiliwa

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo