Wakala wa Tigo Pesa FAQs | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..


Wakala wa Tigo Pesa FAQs

Muamala wa kimakosa utatokea lakini ni muhimu kutoa ripoti mara moja kwa kupiga huduma kwa wateja kwa namba 100. Kama pesa bado haijatolewa bado, Tigo watweza kubadilisha huo muamala na kurudi kwa mteja. Kama pesa imeshatolewa na mpokeaji, mteja atoe taarifa kituo cha polisi na Tigo wataendelea na utaratibu mwingine wa kurudisha pesa.

Cha kwanza  ni kupiga simu kituo cha simu cha Tigo Pesa kwa kupiga 100 au tembelea duka lolote la Tigo Pesa na toa taarifa ya kupotea kwa laini au simu.

Mhudumu atakuuliza maswali ili aweze kuthibitisha uhalisia wa mteja na ndipo kuweza kufunga hiyo akaunti, utaratibu mwingine wa kupata laini nyingine utafuata.

Tigo Pesa inategema mtandao wa Tigo. Kwa bahtai mbaya ambapo mtandao wa Tigo utakua uko chini, epuka kufanya muamala wa aina wowote mpaka pale mtandao utakapo rudi hewani na ukiona simu yako ina mtandao.

Mara nyingi meseji ya kukamilika kwa muamala huingia baada ya muda mfupi lakini kuna muda mwingine mtandao unaweza kusumbua.

Kama umesubiri zaidi ya dakika 10 na hujapata meseji ya kukamilika kwa muamala, angalia salio au piga simu kwa kituo vyetu vya simu kwa kupiga 100.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo