Weekend ofa | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..


 Weekend ofa

Tigo Wikiend Ofa:

Tigo Wikiendi ofa ni kampeni inayo wezesha wateja waliochaguliwa wa malipo ya kabla kupata dakika au MBs za bure wikiendi baada ya kufikia kiwango cha matumizi walichopangiwa katikati ya wiki. (Jumatatu paka Ijumaa).


Mfumo wa Kampeni:

“Tumia katikati ya wiki ufurahie ofa wikiendi” Kila mteja atakuwa na ofa tofauti kulingana na matumizi yake


Ustahiki:

Ofa hii ni kwa wateja wa Tigo wa malipo ya kabla na ni ofa maalum kwa baadhi ya Makundi ya watumiaji kulingana na matumizi yao


Uzinduzi:

Tigo Wikiendi ofa imezinduliwa rasmi tarehe 05 Julai, 2021


Maswali na Majibu:

  Tigo wikiendi Ofa ni nini?

Tigo Wikiendi ofa ni kampeni inayo wezesha wateja waliochaguliwa wa malipo ya kabla kupata Dakika au MBs za bure wikiendi baada ya kufikia kiwango cha matumizi walichopangiwa katikati ya wiki. (Jumatatu paka Ijumaa).

  Nitajuaje nina stahili kupata Tigo wikiendi ofa?

Mteja aliyechaguliwa kwa wiki atatumiwa ujumbe mfupi siku ya Jumatatu unaomjulisha kiwango cha matumizi ya Dakika au MBs anazopaswa kutumia kwa wiki nzima ili kufikisha vigezo vya kupata bonasi ofa a kutumia wikiendi.

  Je hii Tigo Wikiendi Bonasi inaweza ondoa ofa zingine nilizonazo kama Ofay a laini mpya, Longa Nae, Cha Asubuhi?

Hapana, Tigo wikiendi ofa haitoondoa ofa nyingine ambazo zipo kwa ajili yako

  Je ofa hii ni maalumu?

Ofa hii ni maalumu kwa wateja wote wa Malipo ya kabla waliochaguliwa nchi nzima

  Je naweza kupata ofa ya dakika na MBs kwa Pamoja?

Hapana, ofa hii inatolewa kwa Dakika au MBs na sio vyote kwa Pamoja.

  Can the bonus be rollover? Je naweza kubeba ofa hii na kuitumia wikiendi inayofuata?

Hapana, ofa hii itatumika kwa wikiendi iliyopangiwa na itaisha baada ya masaa 48 ya wikiendi hiyo

  Je nitawezaje kujiunga na ofa hii?

Ofa hii haina kuijiunga bali wateja wote waliochaguliwa watapata ujumbe mfupi kila jumatatu kuwajulisha kiwango cha matumizi ya Dakika au MBs wanachopaswa kufanya katikati ya wiki ili kupata bonasi ya kutumia wikiendi

  Je nitajuaje kiwango cha Dakika au MBs nilizozawadiwa kama Bonasi?

Mteja ili kujua kiwango cha Dakika au MBs alizozawadiwa piga *102*00#

Vigezo na Masharti:

 1. Bonus ipo kwa Wateja wa Malipo ya Kabla waliochaguliwa.
 2. Wateja watapata bonasi za Dakika au MBs na sio zote kwa Pamoja
 3. Bonasi inatolewa mara moja tu kwa wiki n ani wikiendi.
 4. Bonasi itatumika tu wikiendi na itadumu kwa masaa 48 (Jumamosi na Jumapili)
 5. Mteja aliyechaguliwa kupata bonasi asipofikisha malengo aliyopewa hatopata bonasi
 6. Mteja yoyote aliyepo ON DEMAND hatochaguliwa kwa ajili ya bonasi
 7. Ujumbe wa kushiriki kupata bonasi utatumwa kama ifuatavyo.
  • Steji 1, utatumwa Jumatatu kumjulisha mteja kiwango cha matumizi ya dakika au MBs anazopaswa kufikia ili kupata bonasi wikiendi.
  • Steji 2, utatumwa Jumatano kumjulisha mteja kiwango kilichobakia ili kutimiza vigezo/malengo.
  • Steji 3, utatumwa ijumaa usiku kumjulisha mteja bonusi aliyopata kutumika wikiendi

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo