Zuia na Ripoti Udanganyifu | Tigo Tanzania

 Zuia na Ripoti Udanganyifu

Ukikutana au kuhisi udanganyifu wa aina yoyote, tafadhali tujulishe haraka iwezekanavo. Kwa bahati mbaya akaunti za pesa za simu za mkononi hutumiwa na majambazi na vibaka. Tigo hatuvumilii udanganyifu wa aina yoyote. Kuhakikisha wateja wetu wanabaki salama, tunajitahidi kufuta akaunti zinazohusishwa na udanganyifu pamoja na kuripoti wahalifu kwa vyombo husika. Kufanya hivyo, tunahitaji msaada wako. Ripoti udanganyifu kwa kupiga 100, au jaza fomu hapo chini.

Njia 10 za Kuzuia Udanganyifu wa Pesa kwenye Simu 

1.       Badilisha namba yako ya siri mara kwa mara.

2.       Kamwe usimshirikishe mtu mwingine namba yako ya siri, au maelezo yako binafsi hata kama akisema ni mwakilishi wa Tigo. 

          a.   Tigo kamwe haitakuomba kutoa namba yako ya siri, ni yako na yako pekee.

3.       Kama akaunti ya Tigo Pesa imehusishwa na akaunti zingine kama simbanking, tumia namba ya siri tofauti kupunguza uwezekano wa udanganyifu.

4.       Kabla ya  kuingiza namba ya siri ili kuthibitisha mumala wowote, hakikisha umehalalisha namba ya unaemtumia.

5.       Pale unapofanya malipo kwa niaba ya mtu mwingine, ni salama zaidi kupokea maelezo ana kwa ana na sio kwa meseji au barua pepe.

6.       Ni salama zaidi kufanya miamala na watu au biashara unaowafahamu na kuwaamini. 

7.       Ukifanya muamala na mtu au biashara usieifahamu, usilipe kabla hujapokea bidhaa ama huduma unayohitaji.

8.       Kamwe usilipe pesa ili kuomba kazi au mkopo. 

          a.   Kama kazi au mkopo inahitaji malipo, inawezekana ikawa ni ya uongo. 

          b.   Thibitisha kwamba gharama ni ya halisi kwa kuangalia vithibitisho rasmi ya shirika kabla ya kulipa. 

9.       Cha muhimu zaidi, tumia busara.

          a.   Kama kitu kinaonekana kizuri sana kua kweli, uliza maswali mengi na endelea kwa tahadhari. 

          b.   Usifanye malipo ya aina yoyote mpaka ukiwa umeridhika kwa asilimia 100 kua muamala ni wa ukweli.

10.     Ikitokea umefanya muamala na ukagundua sio wa kweli, piga 100 haraka iwezekanavyo ili muamala usitishwe.

Ripoti Udanganyifu

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo