Chemsha Bongo | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..

 Chemsha Bongo

Vigezo na Masharti vya Kampeni ya “Chemsha Bongo Trivia”

 1. Vigezo na Masharti:
 • Kila mteja anayeshiriki kampeni hii, anaweza kushinda endapo tu atakusanya pointi nyingi zaidi kwa kujibu maswali mengi pointi nyingi Zaidi ataibuka mshindi. Kwa kila swali atatozwa Tsh100 kwa kila SMS.
 1. Jinsi washindi watakavyo patikana:
 • Washindi wote watapatikana kulingana na wingi wa pointi walizojikunyia kipindi chote cha kampeni kwa kujibu maswali ya Chemsha Bongo.
 • Muwakilishi wa Idara ya Bahati Nasibu Tanzania lazima awepo pindi Mshindi anapotafutwa/kutajwa au kupigiwa simu.
 • Mteja atakavyocheza zaidi ndio anavyozidi kukusanya pointi, na kumuongezea nafasi ya kushinda zawadi nyingi zaidi za Siku,Saa ya maajabu, Wiki na Zawadi kuu itakayotolewa mwisho wa Kampeni.
 • Washindi wote wa Chemsha bongo Trivia watachaguliwa kulingana na pointi walizokusanya. Mteja atakayekuwa amekusanya pointi zaidi ya wengine ndani ya muda wa kutoa Zawadi ndiye atakayechaguliwa kuwa Mshindi.
 1. ZAWADI:
 • Zawadi Kuu:

 Mshindi Mmoja mwenye pointi nyingi zaidi alizokusanya kipindi chote pesa taslimu kiasi cha Tsh 13,000,000 (milioni kumi na tatu)

 • Zawadi Za Kila Wiki:

Kuna Mshindi mmoja kila wiki, Mwenye pointi za juu Zaidi anashinda tsh1,000,000.

 • Zawadi za Siku

Kuna mshindi mmoja wa siku mwenye pointi za juu Zaidi anashinda Tsh 100,000

 1. VIGEZO NA MASHARTI:
 • Mteja anatakiwa ajiunge kwa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571
 • Mteja anaweza pia kucheza kwa kutembelea  http://tigofiesta.co.tz
 • Kila jibu litatozwa Tsh 100
 • Neno lililotumwa kimakosa kwenda 15571 itachukuliwa kama jibu lisilo sahihi kwa swali lililojibiwa. Hivyo utapokea ujumbe kujulishwa na kupewa swali lingine kama mteja atakua na salio.
 • Kila Jibu sahihi la Chemsha bongo Trivia lina pointi 200 na jibu lisilo sahihi lina pointi50.
 • Kampeni itajumuisha maswali yahusuyo muziki na burudani.
 • Kadiri mteja anavyojibu maswali zaidi ndivyo anavyozidi kujiongezea nafasi ya USHINDI kwa kujikusanyia pointi nyingi Zaidi.
 • Kujiondoa kwenye huduma mteja anaweza kutuma neno ONDOA MUZIKI kwenda
 • HAKUNA gharama za kujitoa katika huduma.
 • Mshindi yeyote ambaye alipigiwa simu na hakupatikana au hakujibu simu mara 3 hatokuwa na ruhusa ya kudai zawadi hiyoatapigiwa simu na akipatikana atapewa ushindi.Kwa hiyo mteja mwenye nafasi ya pili.
 • Mshindi yeyote ambaye hatopokea simu au Simu yake Haitopatikana kipindi cha kutangaza Mshindi mara 3 basi nafasi hiyo ITAONDOLEWA kwake na kupewa Mshindi anayefuata mwenye pointi nyingi kupigiwa na akipatikana basi huyo ndio MSHINDI.
 • Zawadi zote za kampeni ya “Chemsha bongo Trivia” zitakabidhiwa katika ofisi za Tigo.
 • Kila mteja ana nafasi ya kushinda zawadi ya KIPENGELE FULANI MARA MOJA (1) tu na hairuhusiwi kushinda kipengele hicho tena. Mfano: Mteja akishinda zawadi ya WIKI ya kwanza, hafai kushinda zawadi ya wiki kwa wiki zinazofuata.
 • Tigo itabakia na zawadi ya Mshindi kwa muda wa miezi mitatu (3) endapo Mshindi huyo hajajitokeza kuichukua zawadi yake. Baada ya muda huo Mshindi hatokuwa na haki ya kuichukua zawadi.
 • Tigo inaweza kutumia baadhi ya taarifa kama picha, sauti au video za MSHINDI aliyeshinda zawadi ya kampeni hii kwa kipindi chote cha kampeni kwa ajili ya uhamasishaji wa kampeni.
 • Jina la Mshindi linaweza kuchapishwa kwenye magazeti au vyombo vingine vya habari.
 • Waajiriwa wa TelcoVAS na Tigo pamoja na familia zao hawana ruhusa ya kushiriki kwenye kampeni hii.
 • Kampeni hii ni kwa ajili ya wateja wote wa Tigo na waishio Tanzania.
 • Majina ya washindi yanaweza kutangazwa au kuchapishwa katika vyombo vya habari vilivyochaguliwa na waendesha kampeni.
 • Washindi wote wanapaswa kutoa vitambulisho halali. Vitambulisho vifuatavyo pia kujumuishwa (Kitambulisho cha NIDA, Kitambulisho cha Kura na Leseni ya Udereva
 • Zawadi zote za Pesa Taslim zitakatwa kodi ya TRA asilimia 20 (20%).
 • Tigo inaweza wa kubadilisha vigezo na masharti muda wowote kwa kupeleka mapendekezo yao katika Taasisi ya Kuratibu Mashindano ya Bahati Nasibu (Gaming Board of Tanzania).

 

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo