Mradi wa Uandikishaji wa Uzazi kwa njia ya simu | Tigo Tanzania
Tafadhali zingatia kanuni za afya nawa mikono na epuka misongamano na endelea kufuatilia kurasa zetu kwa taarifa Zaidi..
 Binafsi

 Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Ufilisi na Udhamini (RITA) na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) kwa pamoja  wanaunga mkono mkakati mpya wa taifa wa usajili  wa uzazi  ambao unaharakisha  usajili mkubwa wa watoto  walio na umri chini ya miaka mitano ili kupata  vyeti vya kuzaliwa. Mfumo huu mpya wa usajili wa uzazi  unatumia mfumo wa ubunifu ulioanzishwa na Tigo.

 Simu ya mkononi  inarahisisha mchakato  wa usajili  wa uzazi  kwa kuingiza  taarifa za  usajili  katika simu ambazo taarifa (data) zinapekewa katika kanzidata kuu  ya RITA kwa wakati sahihi. Matumizi hayo yameundwa ili kufanya kazi katika aina zote za simu  na mifumo  ya uendeshaji.

 Hivi karibuni Malengo Endelevu ya Maendeleo yaliweka wazi  umuhimu wa kusajili kila mtoto anayezaliwa. Kwa mujibu wa  Utafiti wa Afya ya Watu Tanzania (DHS) uliofanyika mwaka 2010 ni asilimia 16 tu ya watoto walio na umri chini ya kika mitano  walikuwa wamesajiliwa  na mamlaka za serikali ambapo kati yao ni asilimia  sita tu walikuwa wamepata vyeti vya kuzaliwa. Hivyo  mkakati huu unalenga  kupambana na changamoto hii ya kuharakisha usajili  wa uzazi wa watoto  na kuanzisha  mfumo ulio na ufanisi  wa usajili wa  uzazi na uraia.

Kwa hali hiyo  mfumo mpya  ni mafanikio makubwa. Katika  mikoa ambayo  usajili ulifanyika yaani Mbeya, Mwanza, Iringa na Njombe  zaidi ya watoto 660,000 walio na umri chini ya miaka mitano walisajiliwa . katika kipindi cha miaka minne  ijayo mfumo huo utapanuliwa na kufikia mikoa  kumi ya ziada ili kuongeza mafanikio. Hatua hiyo  itawezesha kufikisha nusu ya mikoa 31 ya Tanzania kukiwa na uwezo wa kuwafikia takribani watoto milioni nne walio na umri wa chini ya miaka mitano.

 Ubunifu huu  umekuja kipindi ambacho  suluhisho la simu za mkononi  likiwa na  zana muhimu  katika maendeleo hususani  katika Tanzania  kwa kufanya   kupenyeza kwa matumizi ya simu za mkononi  kufikia asilimia 71.

Jiunge kupata majarida yetu ya kila mwezi

Tafuta duka la Tigo