loader image

Graduate Trivia

Vigezo na Masharti vya Kampeni ya “Graduate Trivia” 

 1. Vigezo na Masharti: 
 • Huduma hii ni kwa ajili wa wateja wa Tigo wa malipo ya awali.  
 • Kampeni hii kufanyika kuanzia tarehe 07 Julai 2023 mpaka 06 Oktoba 2023. 
 • Tarehe ya kumalizika kwa kampeni inaweza kubadilika kwa kutegemea muenendo wa utoaji wa Zawadi. 
 • Kila mteja anayeshiriki kampeni hii, anaweza kushinda ila atajiongezea nafasi kubwa ya kushinda endapo tu atakusanya pointi nyingi zaidi kwa kujibu maswali mengi ya Uelewa na maarifa. Kwa kila swali atakalojibu atatozwa Tsh150 kwa kila SMS. 
 1. JINSI YA KUCHAGUA WASHINDI: 
 • Washindi wote wa wiki watapatikana kwa njia ya Droo na Mshindi wa Zawadi Kuu atapewa mwenye pointi za juu zaidi alizojikunyia kipindi chote cha kampeni kwa kujibu maswali ya Maarifa. 
 • Muwakilishi wa Idara ya Bahati Nasibu Tanzania lazima awepo pindi Mshindi anapotafutwa/kutajwa au kupigiwa simu. 
 • Mteja atakavyocheza zaidi ndio anavyozidi kukusanya pointi, na kumuongezea nafasi ya kushinda zawadi nyingi zaidi za Wiki na Zawadi kuu itakayotolewa mwisho wa Kampeni. 
 • Washindi wote wa Graduate Trivia watachaguliwa kulingana na pointi walizokusanya. Mteja atakaye bahatika kati ya washiriki 20 Bora wenye pointi za juu ndani ya muda wa kutoa Zawadi ndiye atakayechaguliwa kuwa Mshindi wa wiki, na Zawadi kuu kwenda kwa mshiriki mwenye pointi za juu alizojikusanyia kipindi chote cha kampeni. 
 1. ZAWADI 
 • Zawadi Kuu:  

 Mshindi Mmoja mwenye Bahati mwenye pointi nyingi zaidi zilizokusanywa kipindi chote cha kampeni atashinda Zawadi Kuu ya TSH 10,000,000. 

 • Zawadi ya kila wiki: (Washindi wa3) 

Mshindi wa Kwanza ni mwenye bahati kati ya washiriki 20 Bora wenye pointi nyingi zaidi zilizokusanywa kipindi chote cha wiki atashinda Zawadi ya TSH 300,000 taslimu anayefatia kwa pointi atapewa Tsh200,000 taslim na wa tatu atapewa Tsh100,000 taslim. 

 

 1. Vigezo na Masharti 
 • Mteja anatakiwa ajiunge kwa kutuma neno GRAD kwenda 15572. 
 •  Mteja anaweza pia kucheza kwa kutembelea  http://tigoquizkitaa.co.tz  
 • Kujiunga ni Bure. Baada ya kujiunga mteja ataanza ujumbe wenye maswali ya maarifa na uelewa. 
 •  Ataghalamia Baada ya kujiunga kikamilifu swali la kwanza atatozwa tsh150 ila swali linalofuata linatolewa bure hadi hapo mteja akijibu swali hilo. 
 •  Neno lililotumwa kimakosa kwenda 15572 itachukuliwa kama jibu lisilo sahihi kwa swali lililojibiwa. Hivyo utapokea ujumbe kujulishwa na kupewa swali lingine kama mteja atakua na salio. 
 • Kila Jibu sahihi la Graduate Trivia lina pointi 200 na jibu lisilo sahihi lina pointi50. 
 • Kampeni itajumuisha maswali ya maarifa na uelewa. 
 • Kadiri mteja anavyojibu maswali zaidi ndivyo anavyozidi kujiongezea nafasi ya USHINDI. 
 • Kujiondoa kwenye huduma mteja anaweza kutuma neno ONDOA GRAD kwenda 15572. 
 • HAKUNA gharama za kujitoa katika huduma. 
 • Mshindi yeyote ambaye alipigiwa simu na hakupatikana au hakujibu simu mara 3 hatokuwa na ruhusa ya kudai zawadi hiyo. Bahati nasibu itafanywa upya kupata mshindi mwingine akipatikana atapewa Ushindi. 
 • Mshindi yeyote ambaye hatopokea simu au Simu yake Haitopatikana kipindi cha kutangaza Mshindi mara 3 basi nafasi hiyo ITAONDOLEWA kwake na kuruhusu mshindi mwingine kutafutwana na akipatikana basi huyo ndio MSHINDI. 
 • Zawadi zote za kampeni ya “Graduate Trivia” zitakabidhiwa katika ofisi za Tigo. 
 • Kila mteja hana nafasi ya kushinda zawadi ya KIPENGELE FULANI ZAIDI YA MARA MOJA (1)Mfano: Mteja akishinda zawadi ya WIKI ya kwanza, akiendelea kucheza kwa bidii hana nafasi nyingine ya kushinda tena zawadi hiyo. 
 • Tigo itabakia na zawadi ya Mshindi kwa muda wa miezi mitatu (3) endapo Mshindi huyo hajajitokeza kuichukua zawadi yake. Baada ya muda huo Mshindi hatokuwa na haki ya kuichukua zawadi. 
 • Tigo inaweza kutumia baadhi ya taarifa kama picha, sauti au video za MSHINDI aliyeshinda zawadi ya kampeni hii kwa kipindi chote cha kampeni kwa ajili ya uhamasishaji wa kampeni. 
 • Jina la Mshindi linaweza kuchapishwa kwenye magazeti au vyombo vingine vya habari. 
 • Waajiriwa wa TelcoVAS na Tigo pamoja na familia zao hawana ruhusa ya kushiriki kwenye kampeni hii. 
 • Kampeni hii ni kwa ajili ya wateja wote wa Tigo na waishio Tanzania. 
 • Majina ya washindi yanaweza kutangazwa au kuchapishwa katika vyombo vya habari vilivyochaguliwa na waendesha kampeni. 
 • Washindi wote wanapaswa kutoa vitambulisho halali. Vitambulisho vifuatavyo pia kujumuishwa (Kitambulisho cha NIDA, Kitambulisho cha Kura na Leseni ya Udereva 
 • Tigo inaweza wa kubadilisha vigezo na masharti muda wowote kwa kupeleka mapendekezo yao katika Taasisi ya Kuratibu Mashindano ya Bahati Nasibu (Gaming Board of Tanzania). 

Tafuta duka la Tigo