loader image

NIVUSHE PLUS 

 


VIGEZO NA MASHARTI

1. MAKUBALIANO

Makubaliano haya yana maelekezo yanayosimamia matumizi ya huduma ya mkopo ya pesa talimu ya Tigo Pesa kama vile Nivushe Plus ambayo inajumuisha mkataba kati yako na huduma ya mikopo ya fedha taslimu ya Tigo Pesa. Vigezo na masharti haya yatatumika kwa mteja mara tu baada ya kujisajili na huduma na yataendelea kutumika katika kipindi chote kutegemea uwepo wa kampuni inayotoa huduma hii ikiwemo usasishaji wake utakaofanyika isipokuwa kama kutakuwapo na usitishawaji wa huduma kutoka upande wowote kulingana na vigizo na masharti haya.

2. MAANA ZA MANENO

2.1. “Makubaliano” inamaanisha vigezo na masharti haya na maagizo mengine au kanuni zingine zozote mahususi (kama vile ombi la manunuzi au agizo la ununuzi) zitakazotumika katika huduma.

2.2. “Ofisi ya Marejeleo ya Mikopo” (Credit Reference Bureau) inamaanisha ofisi ya marejeleo ya mikopo yenye leseni halali chini ya Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania kwa mujibu wa Taratibu za Ofisi ya Marejeleo ya Mikopo ya Benki Kuu ya Tanzania za mwaka 2012, miongoni mwa zingine, kukusanya na kusaidia kupata taarifa za mikopo za wateja.

2.3. “Ada” ina maana ya malipo yote yanayohusika katika huduma na inajumuisha: Kiwango cha riba, ada ya adhabu ya ucheleweshaji, na Ada nyinginezo zozote za mkopo kama zilivyowasilishwa mara kwa mara kwa mujibu wa Mkataba huu na inajumuisha tozo zozote, na kodi zinazotumika chini ya sheria za Tanzania.

2.4. “Kipindi cha Neema” kinarejelea kipindi cha muda maalumu kilichobainishwa ambacho wateja hawaruhusiwi kutozwa ada za kuchelewasha malipo ya mkopo baada ya tarehe ya malipo ya mkopo iliyowekwa.Kipindi cha neema kwa mkopo wa Nivushe Plus kielezwa kuwa ni kipindi cha saa 48 kuanzia tarehe ya mwisho ya Marejesho ya Mkopo. Katika kipindi hiki, hautatozwa ada za ucheleweshwaji wa malipo.

2.5. “Mfahamu Mteja Wako” (Know Your Customer) pia kama ijulikanavyo kama KYC inamaanisha majukumu ya kutambua kikamilifu mteja (Customer Due Diligence) zilizowekwa kwenye Tigo Pesa na sheria zinazohusika na kadri ambavyo itakuwa imeelezwa au kushauriwa na Serikali, Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) au Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mara kwa mara au mamlaka zingine zozote zinazohusika.

2.6. “Nivushe Plus” huduma ya mkopo inayotolewa na Tigo Pesa, ambayo inakupa thamani ya mkopo moja kwa moja kwenye Akaunti yako ya Tigo Pesa.

2.7. “Tigo” ina maanisha kampuni ya MIC Tanzania Limited ambayo umeundwa nchini Tanzania kama kampuni yenye dhima yenye ukomo chini ya Sheria ya Makampuni (Kifungu cha 486 cha sheria za Tanzania)

2.8. “Huduma ya Tigo Pesa” inamaanisha huduma za kuhamisha fedha na huduma za malipo ambazo zinatolewa na Tigo Pesa kupitia mfumo wa Tigo Pesa.

2.9. “Mfumo wa Tigo Pesa” inamaanisha mfumo ambao unaendeshwa na kampuni ya Tigo nchini Tanzania kwaajili ya kutoa huduma za Tigo Pesa kwa kutumia mtandao.

2.10. “Tigo Pesa” inamaanisha hifadhi ya thamani ya fedha katika simu yako ya mkononi, ambayo ni taarifa za kiwango cha fedha zako ulizohifadhi katika mfumo wa Tigo Pesa kwa wakati huo.

2.11. “Mteja wa Tigo Pesa” inamaanisha mtu yoyote aliyesajiliwa kutumia mfumo wa Tigo Pesa kutuma, kupokea au kufanya malipo.au kukamilisha huduma zozote za kifedha zinazotolewa na Tigo Pesa kwa kushirikiana na taasisi ya kifedha.

2.12. “Taarifa Binafsi” maana yake ni taarifa yoyote inayohusiana na mtu wa asilia anayetambulika au anayeweza kutambulika; Mtu anayetambulika ni yule anayeweza kutambuliwa, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa kurejelea namba yake ya kitambulisho au kwa sababu moja au zaidi mahususi kwa utambulisho wake wa mwili, kisaikolojia, kiakili, kiuchumi, kitamaduni au kijamii.

2.13. “Mtoa Huduma” inamaanisha kampuni ambayo itakuwa inatoa huduma hii kwa mteja.

2.14. “Huduma” inamaanisha huduma ya mkopo ya Nivushe Plus.

2.15. “Ada ya kuchelewesha marejesho” ni ada utakayo paswa kulipa baada ya masaa 48 kupita baada ya muda wako wakulipa mkopo kupita muda wake.

2.16. “kurejesha kiasi chote cha mkopo” ni jumla yote ya pesa ya mkopo na gharama zingine zinazo takiwa kulipwa.

3. KUKUBALI VIGEZO NA MASHARTI

3.1. Kabla ya kujisajili na huduma, unapaswa kusoma kwa makini na kuelewa masharti haya ya namna ya utumizi kwa sababu yanasimamia upatikanaji, utumiaji na uendeshaji wa huduma. Masharti haya ya utumizi yanapatikana katika tovuti ya Tigo.

3.2. Iwapo haukubaliani na masharti haya ya utumizi, tafadhali bonyeza “Kataa”.

3.3. Utachukuliwa kuwa umesoma, umeelewa , na kukubali masharti haya ya utumizi: Kwa kubonyeza chaguo la “Kubali” linalokutaka kuthibitisha kwamba umesoma, umeelewa, na kukubali kufuata vigezo na masharti haya; na au kwa kutumia au kuendelea kutumia na kuendelea kuomba huduma.

4. KUJISAJILI NA KUTUMIA HUDUMA

4.1. Ustahikifu

4.1.1. Wateja wa Tigo Pesa wenye akaunti hai za Tigo Pesa ndio watakuwa wanastahili kutumia huduma ya mikopo ya Tigo Pesa.

4.1.2.

4.1.3. Ni wateja ambao wamekuwa wakitumia huduma ya Tigo mara kwa mara na kufanya miamala na Tigo Pesa kwa zaidi ya mwaka mmoja pekee ndio watakaostahili.

4.1.4.

4.1.1. Huduma ya mkopo wa fedha taslim utatolewa kwa namba ambazo zimesajiliwa kwa alama za vidole tu.

4.1.2. Huduma ya Nivushe Plus itatolewa kwa wateja ambao wanastahili kupewa mikopo.

4.1.3. Ustahiki wa kupata mkopo utaamuliwa na Tigo Pesa. Kama ambavyo ilivyoamuliwa na Tigo Pesa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali.

4.2. Utoaji wa huduma ya mkopo ya Nivushe Plus utategemea pointi au alama zinazotolewa na Tigo kwa wakati huo.

4.3. Point au alama za mteja kwaajili ya Nivushe Plus zitasasishwa mara kwa mara kulingana na shughuli za mteja.

4.4. Point au alama za mikopo za mteja zitategemea na mwenendo wa miamala ya mteja katika Tigo Pesa na matumuhizi ya haduma za Tigo.

4.5. Kutegemeana na utendaji wa mteja katika Tigo Pesa na mwenendo wa mkopo wa Nivushe Plus, kiwango cha ukomo wa mkopo kinaweza kuongezeka ua kupungua. Utendaji mzuri utapelekea kukua au kuongezeka kwa kiwango cha ukomo wa mkopo wa Nivushe Plus. Utendaji mbaya utapelekea katika kupungua kiwango cha ukomo wa mkopo wa Nivushe Plus au kuondolewa kabisa kwa kiwango cha ukomo.

4.6. Mteja hataweza kutumia huduma ya mkopo wa Nivushe Plus zaidi ya ukomo aliowekewa.

4.7. Kuanzia siku ya 0-30 hakutakuwa na makato ya moja kwa moja kwenye waleti ya mteja ya Tigo Pesa, mteja anaweza kuchagua kulipa mwenyewe ndani ya siku hizi.

4.8. Katika kipindi cha Neema mteja atatakiwa kurejesha kiasi cha mkopo kilichosalia yeye mwenyewe (kwa mikono). Katika wakati huu, hakuna gharama za ziada, kama vile ada za adhabu za malipo yaliyocheleweshwa n.k. zitakazoongezwa kwenye kiasi cha mkopo wako. Kushindwa kurejesha kiasi cha mkopo wako kilichobakia baada ya kipindi cha neema utatozwa ada za ziada zilizotajwa hapo juu katika kifungu hiki.

4.9. Baada ya kipindi cha Neema kuisha ada za ucheleweshwaji wa malipo na kiasi cha mkopo kilichosalia kitakatwa moja kwa moja katika waleti ya Tigo Pesa ya mteja.

4.10. Ada ya kuchelewesha marejesho itatozwa iwapo utashindwa kurejesha kiasi chote cha mkopo baada ya kwisha kwa kipindi cha Neema.

4.11. Baada ya kuomba huduma ya Nivushe Plus, utapokea ujumbe wa uthibitisho.

4.12. Iwapo haujakidhi vigezo vya kupata huduma ya Nivushe Plus, unapaswa kuendelea kufanya miamalaya Tigo Pesa ili kujenga historia ya miamala na kukuza pointi au alama zako za mikopo (Uwezo wa kukopesheka) ili uweze kustahili.

4.13. Unaweza kuangalia kiawango chako cha mkopo wa Nivushe Plus ulichotengewa kwa kutumia menyu sahihi inayotolewa kwenye kifaa chako kupitia Menyu ya Tigo Pesa na App ya Tigo Pesa na chaneli nyingine yoyote.

4.14. Tunaweza kukupatia kiwango cha chini na cha juu cha mkopo unachoweza kupata katika huduma ya Nivushe Plu; utapata taarifa za viwango hivyo kupitia ujumbe mfupi, Menyu ya Tigo Pesa, na App ya Tigo Pesa, baada ya kuomba.

4.15. Kiwango cha mkopo wa Nivushe Plus kitakuwa kinafanyiwa marekebisho mara kwa mara na tunahaki ya kubadilisha kiwango cha mkopo wa Nivushe Plus kwa kukutaarifu au bila kukutaarifu; ingawa (sio jukumu letu) tutajaribu kukutaarifu mabadiliko yoyote katika mkopo wako wa Nivushe Plus itakapo onekana ni lazima.

4.16. Tigo Pesa na benki washirika na taasisi za kifedha zinaweza kubadilishana taarifa zako binafsi walizonazo kuhusiana na utoaji wa huduma ya Nivushe Plus. Taarifa hizo binafsi zinajumuisha taarifa ambayo zitatuwezesha kukutambua na kutidhi mahitaji ya mamlaka za udhibiti kuhusu “mjue mteja wako”.

5. MAOMBI YA MKOPO

Utakapo omba mkopo, tutakupatia taarifa zifuatazo:

5.1. Kiasi cha fedha ulichoamua kukopa (“Kiwango cha mkopo / Mkopo”).

5.2. Muda kamili wa marejesho ya mkopo unakokotolewa tangu siku ambapo ulipewa mkopo (“Muda wa Mkopo”);

5.3. Jumla ya ada zitaonyeshwa katika skrini yako kama “Ada” na “Asilimia % ya Ada.

5.4. Tarehe ambayo au ambazo unatakiwa kurejesha kiasi chote cha mkopo wako au sehemu ya mkopo inategemea na mkopo wako kama ni wa rejesho moja au una marejesho mengi (Tarehe ya Mwisho);

5.5. Ada ya kutolipa kiasi cha rejesho kufikia siku ya marejesho (“Ada ya kuchelewesha marejesho”) iwapo inahitajika.

5.6. Hauta tozwa ada kubwa zaidi ya ile uliyotajwa wakati wa kuomba mkopo katika kipindi chochote ambacho kiasi cha mkopo wako unabakia kutokulipwa.

6. KUREJESHA YA MKOPO

6.1. Taarifa Muhimu: kwa kukubali Masharti na Kanuni za Mikopo utakuwa umekubali kwamba Tigo inaweza kuruhusu mtoa mikopo kufanya makato ya kiasi cha mkopo kilicho bakia moja kwa moja kwenye akaunti yako ya Tigo Pesa itakapofika siku ya mwisho ya marejesho.

6.2. Ada ya kuchelewesha marejesho itatozwa iwapo utashindwa kurejesha kiasi chote cha mkopo ndani ya siku 2 baada ya kufika kwa siku ya mwisho ya marejesho.

6.3. Iwapo sehemu yoyote ya kiasi cha marejesho kitakuwa hakijalipwa baada ya Siku ya Marejesho kufikia, fedha yoyote ambayo itawekwa kwenye akaunti ya Tigo Pesa kitachukuliwa mpaka kiasi cha mkopo kilichobakia kimerejeshwa chote. Kwa kukubali maelezo hapo juu, unakubali kwamba tunaweza kukata:

6.3.1. Ada ya Kuchelewesha mkopo, na kisha

6.3.2. kiasi cha marejesho (Ambacho hakijalipwa) kiwango unachopaswa kurejesha kwa wakati huo.

7. ADA NA TOZO

7.1. Unawajibika kulipa riba na ada zote zinazohusika katika matumizi ya huduma.

7.2. Riba zote na ada hukatwa kwenye akaunti ya mteja na zinaweza kubadilika wakati wowote kadri tutakavyoona inafaa.

7.3. RIba na ada zinazopaswa kulipwa katika mkopo husika zitatolewa kutoka akaunti yako ya Tigo Pesa Utatulipa na kwa maana hiyo hapa unakubali kwamba tunahaki ya kutoa kutoka kwenye waleti yako ya Tigo Pesa (bila kurejea kwako) riba na ada yoyote ya muamala inayopaswa kulipwa kutegemeana na huduma:

7.4. Isipokuwa utakapo taarifiwa, ada zinajumuisha kodi zote zinazotakiwa zinajumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani, Ushuru wa Bidhaa na kodi nyingine zozote ikiwa ni pamoja na Tozo zinazohusika kwa kiwango cha wakati husika. Kwa hiyo hapa unakubali kulipa ada zote za miamala.

7.5. Malipo yote yanajumuisha kodi yoyote inayopaswa kulipwa kama inavyotakiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

7.6. Kwa hiyo hapa unatupatia sisi ruhusa isiyobadilika ya kufanya marekebisho ya ada kufuatia mabadiliko ya kodi zinazohusika.

8. KUSHINDWA KULIPA MKOPO

8.1. Wakati wowote kutakapo tokea kushindwa kulipwa kwa mkopo tuna haki ya:

8.1.1. Tutasitisha au kubadili mahusiano yetu ya kibiashara na wewe wakati wowote baada yakukujulisha na tunaweza kusitisha huduma ambazo tumeshakupatia na kukutaka kukamilisha malipo ya kiwango cha mkopo kilichosalia ndani ya muda ambao tutakao ona unafaa.

8.1.2. Unaturuhusu kuwasilisha taarifa hizi (ie , tukio la kushindwa kulipa) katika Ofisi ya Maerejeo ya Mikopo kama itakavyokuwa inahitajika au kwa kuendana na Sheria ya Benki au chombo kingine chochote cha udhibiti.

9. ALAMA / POINTI ZA UKOPAJI:

Kiwango cha mkopo wako wa Nivushe Plus na kuendelea kuidhinisha maombi yako ya mkopo yatategemeana na alama / pointi zako za ukopaji. Alama / pointi zako za mkopo zitatathminiwa kutegemeana na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na taarifa zilizopatikana kutokana na matumizi yako ya Huduma za Tigo na Tigo Pesa, na historia ya marejesho ya kiwango cha kikomo chako cha Nivushe Plus.

10. MATUMIZI YA TAARIFA ZAKO

10.1. Tutatumia taarifa zako binafsi kama ilivyoelekezwa katika namna ambayo inakubaliwa na sheria..

10.1.1. Unapokubali Kanuni na Masharti, unakubali kwamba taarifa kibinafsi zinaweza kutumika kutathmini iwapo tunaweza kukupatia kiasi cha mkopo. Inajumuisha namba yako ya simu, jina lako na jina lako la ukoo, tarehe ya kuzaliwa, kitambulisho au namba ya hati ya kusafiria na taarifa zote kuhusu akaunti yako ya Tigo Pesa na jinsi unavyoitumia na taarifa zilizoko katika maombi yako ya mkopo.

10.1.2. Vile vile unakubali na kuturuhusu kupata, kutoa taarifa na kutumia taarifa zako binafsi na taarifa za matumizi ya mkopo wa Nivushe Plus. Hii ni pamoja na kutoa taarifa hizi kwenda kwenye Ofisi ya Marejeleo ya Mikopo (miongoni mwa mengine) kufanya ukaguzi wa mikopo au kuripoti kwenye Ofisi ya Marejeleo ya Mikopo kama inavyoweza kuwa desturi ya soko au inavyotakiwa na sheria na wahusika wengine, ikiwepo Mtoa Huduma, kama inavyoidhinishwa chini ya sheria zinazohusika.

10.2. Kwa hiyo hapa unakubali bayana na kuidhinisha sisi kutoa, kupokea taarifa au kutumia taarifa zako binafsi au taarifa au takwimu zinazohusiana na akaunti yako ya Tigo Pesa na huduma zingine za Tigo Pesa kufuatia huduma ya mkopo uliyopewa na taarifa zingine zozote za matumizi ya huduma:

10.2.1. Kwa madhumuni mema ya kibiashara kuendana na utumizi wako wa huduma, kama vile masoko na uchunguzi kuendana na shughuli; na

10.2.2. katika utendaji wa kibiashara ikiwemo lakini bila kuwa na ukomo katika udhibiti wa viwango, mafunzo na kuhakikisha ufanisi wa mifumo.

10.2.3. Unatupa idhini sisi kutoa taarifa yoyote kuhusu Tigo Pesa akaunti kwa chombo chochote cha sheria cha ndani au cha kimataifa au asasi za kiserikali ili kusaidia kuzuia, kugundua, kufanya uchunguzi au mashtaka ya vitendo vya jinai au wizi au kwa taasisi nyingine zozote au mtu wa tatu kama inavyotakiwa na sheria ya nchi yoyote na kama tutakavyoona kuwa ni muhimu.

10.3. Unatupa idhini ya kutoa, kujibu, kushauri mabadilishano na kuwasilisha taarifa zinazohusiana na akaunti yako ya Tigo Pesa na au mkopo wako kwa mtu taasisi nyingine inayohusika katika usimamizi wa Akaunti yako ya Tigo Pesa na mkopo, kusasisha hifadhi yetu ya taarifa, au kutoa msaada kwa mtumiaji.

11. KUSITISHA, KUBADILI NA KUSIMAMISHWA

11.1. Wakati wowote tunaweza kusitisha au kubadilisha mahusiano yetu ya kibiashara na wewe na kusimamisha au kusitisha usajili wako na au kusitisha huduma kwako.

11.1.1. Iwapo unatumia huduma au mkopo katika mambo ambayo hayajaidhinishwa au pale ambapo tunabaini matumizi yoyote mabaya, ukiukwaji wa makubaliano yaliyomo humu, wizi au jaribio la kuiba kuhusiana na utumizi wa huduma.

11.1.2. Iwapo akaunti yako ya Tigo Pesa au makubaliano ya Tigo au Tigo Pesa yatakuwa yamesitishwa kwa sababu yoyote.

11.1.3. Iwapo tutatakiwa au tutaombwa kutii agizo au maelekezo ya au mapendekezo kutoka serikalini, mahakamani, Vyombo vya udhibiti au mamlaka zinazohusika kufanya hivyo au kulazimu kufanyika hivyo.

11.1.4. Iwapo kwa sababu za wazi tunatilia mashaka au tunaamini kwamba umekiuka vigezo na masharti haya ya utumizi (ikiwemo kutolipa kiwango chochote kilichobakia pale inapohitajika).

11.1.5. Pale ambapo akaunti yako ya Tigo Pesa inapokuwa haiko hai au haifanyi kazi kwa muda mrefu au kuonekana kuwa imeondolewa.

11.1.6. Iwapo tutakuwa tumesimamisha utoaji wa huduma au kuacha kutoa huduma kwa sababu za kibiashara au kwa sababu zingine zozote tutakazoona zinafaa.

11.2. Unaweza kusitisha na kujitoa kwenye usajili wa huduma wakati wowote kupitia kifaa chako; Hata hivyo hautaweza kusitisha usajili iwapo una mkopo ambao haujalipwa, kiwango cha fedha kilichobakia, au ada ambayo haijalipwa.

11.3. Usitishaji hautaathiri haki zako zilizolimbikizwa na dhima ya pande zote na hususani hazita athiri majukumu yako ya kutekeleza dhima yoyote iliyopatikana kabla ya usitishwaji.

11.4. Tunaweza kusitisha mahusiano na wewe na kuzuia upatikanaji wa huduma kwako iwapo utashindwa kulipia mkopo kikamilifu pamoja na ada zote ambazo hazijalipwa ndani ya kipindi cha mkopo.

12. MABADILIKO NA MABORESHO

12.1. Tunaweza kuongeza, kuboresha , au kubadili hivi vigezo na masharti ya matumizi wakati wowote tutakapoona inafaa..

12.2. Tunaweza kubadilisha ada na tozo au kuongeza au kupunguza ada zilizopo na kubadili wakati wowote; kutokana na sababu za moja kwa moja za sheria, vyombo vya kisheria, kanuni na miongozo ya Serikali au leseni, kutambulishwa au kubadilishwa kwa kodi za serikali au kama matokeo ya kufanya marekebisho ya mipango ya kibiashara ya Tigo Pesa, mabadiliko ndani ya sekta, mapendekezo kutoka kwenye vyombo vya udhibiti au sababu zingine kama itakavyokuwa inahitajika.

12.3. Tutajaribuku kukufahamisha kabla iwapo tunaongeza au kubadilisha masharti haya ya utumizi. Kiasi na aina ya taarifa tutakazo kupatia zitafuata mfumo muhimu uliopo na unaopatikana kwa wakati huo. (Kwa mfano, tunaweza kukupa taarifa kwa ujumbe wa barua pepe, simu (ikiwemo ujumbe uliorekodiwa au ujumbe mfupi) au kwa tangazo katika gazeti la kila siku au la kila wiki au katika tovuti yetu au kupitia mitandao ya kijamii au kwa njia nyingine yoyote). Mabadiliko yatatokea kabla au baada ya kukupa taarifa, unashauriwa vile vile kutembelea tovuti yetu mara kwa mara kuangalia mabadiliko kusudi ikitokea kwa sababu zisizofahamika ukawa haukupata ujumbe wa mabadiliko.

13. WAJIBU WA KULINDA TAARIFA ZAKO NYETI

Unakubali kwamba utawajibika kulinda na kutumia kwa usahihi simu yako ya mkononi na kuhifadhi namba yako ya siri ya Tigo Pesa inayotumika katika kaunti yako kwa siri na kwa usalama. Utahakikisha kwamba namba yako ya siri ya Tigo Pesa haijulikani au kutambuliwa na mtu yoyote bila idhini yako. Hatutawajibika iwapo utatoa namba yako ya siri ya Tigo Pesa kwa mtu mwingine yoyote na matokeo yake ikapelekea hasara kwako.

14. HAKUNA DHIMA

Tigo Pesa au taasisi za kifedha washirika hazitawajibika kwa hasara yoyote au uharibifu, utakaosababishwa au unaohusiana na maombi yako au matumizi ya mkopo wa Nivushe Plus.

15. KWA UJUMLA

Iwapo msuluhishi aliyeteuliwa kisheria, mahakama au vyombo vya usimamizi (vyenye mamlaka) vitakuta kuwa utoaji wa kanuni na vigezo hivi kuwa batili au visivyotekelezeka, haitaathiri mashati na vigezo vingine.

16. SHERIA ZINAZOSIMAMIA

Malalamiko yote au utofauti utakaotokana au utakaohusiana na mkopo huu kwa njia ya simu ya mkononi vitatatuliwa kwa mujibu wa taratibu za mahakama ya Tanzania

17. MALALAMIKO NA MCHAKATO WA UTATUZI

17.1. Kwa msaada wa aina yeyote kutoka Tigo, Piga 100 (Huduma kwa Wateja). Kwa taarifa zaidi kuhusu kurejesha mwamala, tembelea http://www.tigo.co.tz/tigo-pesa/self-care

17.2. Katika hali ambayo kitengo cha Huduma kwa Wateja hawakuweza kukusaidia na unataka kupeleka mbele suala lako kwenda complain@tigo.co.tz eleza wazi suala lako na wapi lilikotokea.

17.3.Katika hali ambayo haukuridhika na huduma za Tigo kwa Ujumla au suala lako bado halijatatuliwa baada ya Uongozi wa Tigo kuingilia kati, unashauriwa kuwasiliana na TCRA au BOT

Tafuta duka la Tigo