loader image

ISHIKISTAA

Vigezo na Masharti vya Kampeni ya “ISHIKISTAA SMS TRIVIA PROMOTION 

  • Vigezo na Masharti: 
  • Huduma hii ni kwa ajili ajili wa wateja wa Tigo wa malipo ya awali. 
  • Kampeni hii itafanyika kwa muda wa miezi mitatu (Miezi 3) 
  • Tarehe ya kumalizika kwa kampeni inaweza kubadilika kwa kutegemea muenendo wa utoaji wa Zawadi. 
  • Kila mteja anayeshiriki kampeni hii, anaweza kushinda endapo tu atakusanya point nyingi Zaidi kwa kujibu maswali ya mpira na kuingia kwenye droo. Kila swali mteja atakalojibu atagharamia Tsh 99. 
  • Washiriki wote wa kampeni hii ni lazima wawe na miaka 18 na Zaidi. 
  • Mteja anaweza kujiunga kwenye huduma kwa kutuma neno STAA kwenda 15633. Kujiunga ni bure na baada ya hapo mteja atapokea maswali yanayouhusu Wasanii. Kila swali atakalopokea litamgharimu Tsh 99. 
  • Neno lolote ( isipokuwa A au B) litakalotumwa kwenye namba 15633 litajumuishwa kama jibu lisilo sahihi kwa swali lililopita. Mfumo utatuma SMS ya swali linalofuata kama mteja ana salio la kutosha. 
  • Kila jibu sahihi mteja atapokea point MIA MOJA (100) na lisilo sahihi mteja atapokea point Ishirini na tano (25) 
  • Ili kupata nafasi ya kushinda, mteja anapaswa kujibu maswali ya wasanii kuongeza nafasi yake ya ushindi. 
  • Washiriki wote wanaweza kupokea swali la awali muda wowote wa siku pindi watakapokuwa na salio kwenye simu zao ili kuwahimiza kucheza na kupata nafasi ya kushinda zawadi. 
  • Auto-renewal inamaanisha kila siku mteja atatozwa kiasi flani bila kutaarifiwa kwajili ya kubakia kwenye huduma. Mteja atazawadiwa nafasi ya kujibu swali 1 bure na asipotumia nafasi hiyo kwa siku husika hakuna pande ya kulaumiwa. 
  • Mteja anapojibu maswali mengi zaidi ndio anajiongezea pointi na anapata nafasi ya kujiongezea USHINDI. 
  • Washiriki wote wa kampeni wana nafasi sawa ya KUSHINDA, Ukijibu Zaidi ndio unajiongezea nafasi ya KUSHINDA kwenye kila droo. 
  • Kujitoa katika huduma mteja anatakiwa kutuma neno ONDOA STAA kwenda 15633. 
  • HAKUNA gharama za kujitoa katika huduma. 
  • Mshindi yeyote ambaye hatopokea simu/ Simu yake Haitopatikana kipindi cha kujulishwa Mshindi mara 3 basi nafasi hiyo ITAONDOLEWA kwake na droo nyingine kufanyika ili kumchagua mshindi mwingine. 
  • Mshindi yeyote ambaye alipigiwa simu na hakupatikana/ hakujibu simu mara 3 hatokuwa na ruhusa ya kudai Zawadi hiyo. 
  • Zawadi zote za kampeni ya “ ISHIKISTAA SMS TRIVIA PROMOTION” zitakabidhiwa katika office za Tigo. 
  •  Kila mteja ananafasi ya kushinda Zawadi ya KIPENGELE FULANI MARA MOJA (1) tu na hairuhusiwi kushinda kipengele hicho tena. Mfano. Mteja akishinda Zawadi ya WIKI ya kwanza, hafai kushinda Zawadi ya wiki kwa wiki inyofuata. 
  •  Tigo itabakia na Zawadi ya Mshindi kwa muda wa miezi mitatu (3) endapo Mshindi huyo hajajitokeza kuichukua Zawadi yake. Baada ya muda huo Mshindi hatokuwa na haki ya kuichukua Zawadi.  
  •  Tigo inaweza kutumia baadhi ya taarifa kama picha, sauti au video za MSHINDI aliyeshinda Zawadi ya kampeni hii kwa kipindi chote cha kampeni kwa ajili ya uhamasishaji wa kampeni. 
  • Jina la Mshindi linaweza kuchapishwa kwenye magazeti au vyombo vingine vya habari.  
  • Waajiriwa wa Green Telecom na Tigo pamoja na familia zao hawaruhusiwi ya kushiriki kwenye kampeni hii. 
  • Kampeni hii ni kwa ajili ya wateja wote wa Tigo ambao ni raia wa Tanzania. 
  • Majina ya washindi yanaweza kutangazwa au kuchapishwa katika vyombo vya habari vilivyochaguliwa na waendesha kampeni. 
  •  Hakutakuwa na Makato ya ushuru kwenye zawadi za pesa zinazotolewa. 
  •  Zawadi katika kampeni hii hairuhusiwi kubadilishana, kubadilishwa kwa kupewa mtu mwingine. 
  • Washindi wote wanapaswa kutoa vitambulisho halali. Vitambulisho vifuatavyo kujumuishwa ( Kitambulisho cha NIDA, Kitambulisho cha mpiga Kura au Leseni ya Udereva)  
  • Tigo inauwezo wa kubadilisha vigezo na masharti muda wowote kwa kupeleka mapendekezo yao katika Taasisi ya Kuratibu Mashindano ya Bahati Nasibu (Gaming Board of Tanzania) 

 

  • Jinsi ya kuchagua washindi: 
  • Kila wiki zawadi zitatolewa kwa washindi baada ya kushiriki kwenye kampeni kwa kupitia namba husika ya SMS (15633) na kukusanya point Zaidi na kuingia kwenye droo. 

 

  • Muwakilishi wa Idara ya Bahati Nasibu (Gaming Board) lazima awepo pindi Mshindi anapotafutwa/kutajwa au kupigiwa simu. 
  • Kila unavyozidi kujibu maswali ndio unayojiongezea point na nafasi ya kuingia kwenye DROO. 
  • Mshindi wa wiki atakuwa ni yule atakaebahatika kati ya namba 50 zilizokusanya alama nyingi katika wiki na kufanyiwa droo ya ushindi 
  • Mshindi wa Msimu ni yule atakaebahatika kati ya namba 20 zilizokusanya ALAMA nyingi Zaidi kwa kipindi cha Msimu Mzima (Siku 90) na kufanyiwa droo. 

 

  • ZAWADI; 
  • ZAWADI YA MWISHO WA MSIMU:  

Kutakuwa na Mshindi mmoja (1) wa zawadi  ya mwisho wa msimu, ambaye atashida Tsh 2,000,000 (Milioni Mbili tu).  

 

  • ZAWADI ZA WIKI: 

Kutakuwa na Mshindi mmoja kila wiki katika kipindi chote cha msimu ambae atashinda kiasi cha Tsh 200,000 (Laki Mbili tu).  

  • ZAWADI ZA SIKU: 

Kutakuwa na Washindi watatu (3) wa Tsh 10,000 na washindi Kumi (10) wa Tsh 5,000 kilasikua kwa jumla ya siku 90. 

 

Mshindi atatangazwa kwa umma ndani ya siku tatu (3) za kazi. 

4.UPATIKANAJI WA TAARIFA MUHIMU WA KAMPENI 

  • Taarifa zote muhimu kuhusu kampeni zinaweza kupatikana katika tovuti rasmi ya mtandao wa Tigo na kurasa zake za kijamii Pamoja na kurasa maalum ya kijamii ya Soka. 
  • Instagram: sokaupdate 
  • Facebook: sokaupdate 
  • Website: tigo.co.tz 
  • Endapo kampeni itafika mwisho, wahusika wa kampeni watatoa taarifa rasmi kwa wateja kupitia vyanzo rasmi vya taarifa na wateja watapokea ujumbe mfupi. 
  • Usitishwaji au ukatizwaji wa kampeni hakumpi nafasi mtoa huduma ya kuyaacha majukumu yake ya kutoa zawadi zilizokwisha tangazwa isipokuwa pindi tu Usitishwaji au ukatizwaji wa kampeni uko nje ya uwezo wa mtoa huduma. 
  • Mtoa huduma wa Kampeni hana ruhusa ya kutoa taarifa yoyote ya washiriki wa mchezo ISIPOKUWA ikihitajika kufanywa hivyo kisheria. 
  • Mtoa huduma ana haki ya kutoingia kwenye mazungumzo ya maandishi au kuwasiliana na washiriki isipokuwa kwa mujibu wa Kanuni na Masharti au kwa mujibu wa mahitaji ya sheria Tanzania ya sasa. 

 

  • Ni wajibu kwa mtoa huduma kuhakikisha namba ya huduma “short code” inapatikana/inafanya kazi kwa kipindi chote cha kampeni. 

 

 

  • UKOMO WA KUPOKEA TAARIFA ZA MCHEZO/KAMPENI  

Taarifa zote za mchezo kupokea mwisho wa siku saa 5:59:59. 

  • 6. KUSITISHWA KWA HUDUMA AU MASHARTI YA MATUMIZI

Endapo kutakuwa na usitishwaji wa huduma au moja ya matumizi ya masharti kwa hiyari yetu, taarifa inaweza kutolewa kwenu kwa kupitia barua, barua pepe, kupigiwa simu (Kwa ujumbe uliorikodiwa au ujumbe mfupi sms) kupitia machapisho ya kila siku au ya kila wiki au kuchapishwa kupitia tovuti yetu rasmi. Unashauriwa kutembelea tovuti yetu mara kwa mara iili kuengalia kama kuna machapisho ya mabadiliko yeyote ambayo yanaweza kutowafikia kwa matatizo ambayo yapo nje ya uwezo. 

Tafuta duka la Tigo